Mahakama za Nakuru zimetakiwa kuhakikisha kesi za watoto zinashughulikiwa kwa muda ufaao. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Afisa msimamizi wa rumande ya watoto kaunti ya Nakuru Bi Lorna Sang anasema kuwa kumekuwa na kujikokota namna kesi za watoto zinavyoshughulikiwa.

Anasema kesi za watoto zafaa kushughulikiwa katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. 

"Katika rumande hii, kwa mujibu wa sheria watoto hawafai kukaa kwa zaidi ya miezi mitatu, lakini ndivyo ilivyo kwani kesi zao zinapelekwa polepole," alisema Sang.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa wazazi na jamii kwa jumla kujali maslahi ya watoto.

Alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya kipekee na mwandishi huyu wa habari. 

 Picha: Lorna Sang, afisa wa rumande ya watoto Nakuru. Ametaka idara ya mahakama kushughulikia kesi za watoto kwa muda unaofaa. PMambili/Hivisasa.com