Afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma imeitaka Mahakama ya Mombasa kutumia ushahidi wa mtoto aliyefariki kwenye kesi ya ulawiti.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Upande wa mashtaka umeiomba mahakama kukubali kutumika kwa nakala za ushahidi za mtoto huyo wa miaka 13, aliyefari baada ya kulawitiwa.

Mtoto huyo aliandiksha nakala hizo katika kituo cha polisi cha Makupa mnamo mwaka jana, siku chache baada ya kulawitiwa.

Afisi ya mwendesha mashtaka imesema mtoto huyo ambaye ni shahidi na mlalamishi kwenye kesi hiyo, aliaga dunia mwezi Mei mwaka huu, hii ikiwa ni takriban mwaka mmoja baada ya kulawitiwa.

Jamali Salim Mohamed, Hassan Kadegere na Daudi Mwachiro wanakabiliwa na madai ya kumlawiti mtoto huyo katika eneo la Ganjoni mwezi Oktoba, mwaka 2015.

Kesi hiyo itasikizwa siku ya Jumatano mbele ya Hakimu Henry Nyakweba.