Mkurugenzi mkuu wa KPA amepata afueni baada ya mahakama kuu ya Mombasa kufutilia mbali agizo la kumtaka kufika kizimbani kujibu shtaka la ukiukaji wa agizo la mahakama.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wiki mbili zilizopita, mahakama kuu ilikuwa imemwagiza mkurugenzi huyo, Catherine Muturi, kufika mahakamani ili kuweka wazi kwanini alikiuka agizo la mahakama kwa kusimamisha shughuli za mabohari yanayomilikiwa na familia ya Gavana wa Mombasa Hassan Joho, licha ya mahakama kuagiza kutofungwa kwa mabohari hayo.

Hatua hii inaajiri baada ya KPA kuwasilisha ombi la dharura mbele ya Jaji Mathew Emukule, la kutaka mkurugenzi huyo, Catherine Muturi, kutofikishwa mahakamani.

Wakili wa KPA Billy Kongore aliambia mahakama kuwa KPA wanafanya majadiliano na wamiliki wa mabohari hayo ili kesi hiyo kusikilzwa na kuamuliwa nje ya mahakama.

Jaji Emukule alikubali ombi hilo siku ya Jumanne na kuagiza kutofika mahakamani kwa mkurugenzi huyo.