Jengo la Mahakama ya Mombasa. Picha: Haramo Ali/ hivisasa.comMahakama ya Mombasa imewaondelea wana wa Akasha mashtaka ya kuzua fujo na utumizi mbaya wa bunduki.Hakimu Henry Nyakweba amewaondelea mashtaka Baktash Akasha na Ibrahim Akasha walio nchini Marekani kujibu mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.Hata hivyo, kesi hiyo itaendelea kwa upande wa bwanyenye Ali Punjan.Wana hao wa Akasha pamoja na Ali Punjan wanadaiwa kuzua vurugu na kutumia bunduki vibaya katika mkahawa mmoja eneo la Nyali mnamo Januari Mosi mwaka huu.Hapo awali, wakili wa Punjan Francis Kadima aliitaka mahakama kutupilia mbali kesi dhidi ya mteja wake akidai kuwa kesi hiyo haina uzito wowote kwa sababu watuhumiwa wengine wanaokabiliwa na shtaka sawia na hilo wanakabiliwa na mashtaka ya ulanguzi ya dawa za kulevya nchini Marekani.Kesi hiyo itatajwa mnamo Aprili 24 mwaka huu.

Share news tips with us here at Hivisasa