Idara ya Mahakama pamoja na afisi ya mkurugenzi mkuu ya mashtaka ya umma zimetakiwa kuharakisha kusikiliza kesi za ufisadi zinazowakabili wanasiasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Afisa kutoka shirika la Haki Afrika, Francis Auma, amesema itakuwa bora kwa kesi hizo kumalizwa kabla ya kampeni za uchaguzi kupamba moto.

“Itakuwa bora iwapo kesi za ufisadi zitamalizwa kabla ya uchaguzi ujao, ili Wakenya wawajue viongozi wafisadi mapema,” alisema Auma.

Auma ameitaka mahakama kuwachukulia hatua viongozi watakaopatikana na hatia za ufisadi, ili wasiweze kuchaguliwa tena katika uchaguzi ujao.

“Wanafa kuhukumiwa iwapo watapatikana na hatia, angalau ufisadi upungue,” alisema Auma.

Aidha, afisa huyo amewasihi Wakenya kutowachagua wanasiasa wanaokabiliwa na visa vya ufisadi.

Haya yanajiri huku kesi nyingi za ufisadi zikiendelea kusikizwa katika mahakama mbali mbali kote nchini.