Idara ya Mahakama imetakiwa kutembelea maeneo ya matukio kabla ya kutoa maagizo ya ubomozi wa nyumba za wananchi.
Akizungumza siku ya Jumatano wakati wa maadhimisho ya sherehe za Madaraka katika uwanja wa Tononoka, Kaunti kamishna wa Mombasa Mohamed Maalim alizitaka mahakama kuwa na ufahamu mwafaka kuhusu nyumba ambazo wanaagiza kubomolewa hasa kwenye mizozo ya ardhi jijini Mombasa.
“Wananchi wengi wamekuwa wakiachwa bila makao baada ya nyumba zao kubolewa pindi tu mahakama inapotoa uamuzi huo pasi kujali idadi ya wananchi watakao athirika,” alisema Maalim.
Kauli hii inajiri baada ya majumba mengi kubomolewa jijini Mombasa hasa kufuatia mizozo ya ardhi.