Shughuli za kawaida katika afisi za wizara ya afya mjini Naivasha zimetatizika mapema Jumanne Aprili 12, baada ya genge la majambazi kudaiwa kuvamia eneo hilo na kuiba talakilishi tano.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bado haijajulikana idadi ya majambazi hao lakini mashine walizoziiba zilikuwa na habari muhimu ya serikali.

Mkuu msimamizi wa wizara hiyo wilayani Naivasha Dkt Oren Ombiro amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa walikuwa wamewaarifu polisi kuhisiana na wizi huo.

"Tunashirikiana na polisi ili kuweza kuangalia kamera za CCTV kama njia moja ya kufanya uchunguzi wetu," aliongeza Bw Ombiro.

Tukio hilo limesambaratisha shughuli eneo hilo huku maafisa wa wizara hiyo wakikosa mashine za kufanyia kazi kufuatia tukio hilo la usiku wa kuamkia leo.