Serikali ya Kaunti ya Mombasa imeweka mikakati ya kupiga rangi majumba yote ya mji huo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katibu wa Kaunti ya Mombasa Bwana Francis Thoya amesema kuwa wameweka mikakati hiyo kama njia moja ya kubadilisha sura ya mji huo, pamoja na kuboresha viwango vya utalii katika kaunti.

Bwana Thoya alisema kuwa watafanya kikao na washikadau na wafanyabiashara wanaomiliki majumba mjini, ili kujadili namna ya kufanikisha mradi huo.

“Kwa ushirikano na Idara ya Uchukuzi na ile ya Ardhi, Mipango na Nyumba, tutatoa notisi hivi karibuni kuwashauri washikadau kuchukua jukumu la kupiga majengo yao rangi,” alisema Thoya.

Katibu huyo alisema kuwa ipo haja ya kuregesha hadhi ya mji wa Mombasa, kwa kuwa majumba mengi ni makuukuu na hayajafanyiwa ukarabati kwa zaidi ya miaka kumi.