Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC Isaack Hassan amesema kwamba hatong’atuka afisini licha ya shinikizo za muungano wa Cord.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza siku ya Jummane alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu sheria, Hassan alisema kuwa maandamano yanayoandaliwa na Cord hayawezi kuwaondoa maafisa wa IEBC afisini kwani wanahuduma kikatiba.

Aidha, Hassan alishikilia msimamo wake kuwa sharti sheria ifuatwe kabla kubanduliwa kwa IEBC kwani tume hiyo ilibuniwa kisheria.

Hata hivyo, Hassan aliimbia kamati hiyo kuwa wako tayari kwa mazungumzo na serikali na upande wa upinzani ili kusuluhisha masuala tata kabla kuelelekea kwa uchaguzi mkuu wa 2017.

Kwa majuma matatu sasa, muungano wa upinzani Cord umeandaa misururu ya maandamano kushinikiza tume ya IEBC kubanduliwa huku vinara wake wakieleza kukosa imani na tume hiyo.