Padri Joseph Wainaina wa kanisa katoliki dayosisi ya Nakuru ametoa wito kwa wazazi na hasa akina mama kuwapa malezi bora watoto wao ili wawe na mwelekeo pasina kujiingiza katika maswala ya uhalifu. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza Jumamosi katika shule ya upili ya Nakuru kutwa wakati wa mkutano maalumu wa kina mama wakatoliki, Padri Wainaina alisema kuwa akina mama wanafaa kuwalea watoto katika njia za kurejesha hadhi Nakuru. 

Aliongeza kuwa akina mama pia wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa kisiasa.

"Tunajua wanasiasa Kwa sasa wanaendelea na siasa na ni vyema kuwaombea ili wawe na hekima," alisema Padri Wainaina.

Wakati huo huo, alitoa wito kwa wakenya kushirikiana na taasisi ya kupambana na ufisadi ili kuhakikisha swala hilo linatokomezwa. 

Alisema kuwa vita dhidi ya ufisadi havitafaulu iwapo taasisi moja itaachiwa pekee kushughulikia swala hilo. 

Picha: Padri Joseph Wainaina wa kanisa katoliki dayosisi ya Nakuru. Ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha malezi bora Kwa watoto wao.PMambili/Hivisasa.com