Mali ya mamilioni ya fedha imeripotiwa kuharibika baada ya mkasa wa moto kuzuka katika eneo la Kona Mpya eneo bunge la Likoni.

Share news tips with us here at Hivisasa

Moto huo unaripotiwa kuteketeza nyumba yenye vyumba 13, mwendo wa saa mbili asubuhi siku ya Alhamisi.

Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.

Maafisa wa zima moto kutoka serikali ya Kaunti ya Mombasa pamoja na jeshi la wanamaji la Mtongwe hawakufanikiwa kuzima moto huo baada ya kukosa njia ya kufika kwenye nyumba hiyo.

Hakuna aliyeripotiwa kuumia katika mkasa huo.