Wafanyibiashara wamepata hasara kubwa leo katika mji wa Kisii kutokana na vurugu kati ya wanafunzi wa taasisi ya Gusii na maafisa wa polisi.
Wakiongea katika kituo cha magari, wanabiashara hao wameghadhabishwa na jinsi watu wamepora mali yao kutokana na vurugu kati ya wanafunzi na maafisa wa polisi.
Maafisa hao walifika ili kudumisha usalama, lakini wanafunzi waliwarushia mawe jambo lilopelekea wanafunzi kufurushwa hadi katikati mwa mji wa Kisii walipopora mali ya wafanyibiashara hao.
Wafanyibiashara hao wameeleza kuwa hawakufurahishwa na jinsi maafisa hao wa polisi walifanya shughuli hiyo ya kuweka usalama kwa kusema kuwa maafisa hao hawakustahili kuwafurusha wanafunzi hao mpaka katikati mwa mji jambo lililopelekea kuporwa kwa mali yao.
Kati ya mali iliyoporwa ni simu za mikono ,tarakilishi kutoka kwa duka moja karibu na duka la jumla la Tuskys.
Iliwabidi wafanyibiashara wengine kufunga duka zao mapema ili kujingika kutokana na waporaji hao.
Wafanyibiashara hao wamewalaumu watoto wanaorandaranda mjini ambao walionekana kuwa mstari wa mbele katika uporaji huo na kuiomba serikali ya kaunti ya Kisii kuwatoa watoto hao mijini.
Mali hiyo ilianzwa kuporwa hapo jana jioni wakati walipora na kuharibu kituo cha mafuta.
Mali ya dhamani kubwa iliporwa ikiwemo mafuta waliyotumia kuchoma gari lililofanya ajali hiyo ya jana.
Waliokuwa wanasafiri walikwama kwa muda kutokana na wenye magari kuyatoa magari yao kwa kuhofia kuchomwa kwa magari hayo.
Haya yote ni kutokana na gari moja kuwauwa wanafunzi wawili wa taasisi ya Gusii jana jioni karibu na kiingilio cha taasisi hiyo jambo lililowapelekea wanafunzi hao kujawa na ghadhabu kwa kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na afisa wa polisi .