Jaji Patrick Otieno, wa Mahakama kuu ya Mombasa amezuia benki ya Imperial kuwalipa wateja wake pesa zao kwa awamu, hadi kesi iliyowasilishwa na mfanyibiashara wa Mombasa kutaka walipwe pesa zao kwa awamu moja kusikizwa na kuamuliwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mahakama iliambiwa siku ya Jumanne kuwa benki ya Imperial ilikua imeamua kumlipa mfanyibiashara Ashok Doshi, shilingi milioni moja kila mwezi, hadi atakapolipwa shilingi bilioni moja anazodai benki hiyo.

Wakili wa mfanyibiashara huyo, Francis Kadima, alisema kuwa mteja wake hakuhusishwa katika uamuzi wa benki hiyo.

Aidha, aliikosoa Benki Kuu ya Kenya CBK, kwa kuacha benki hiyo kuhudumu kwa muda mrefu bila uangalifu.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 5 mwezi Mei.