Jengo la mahakama ya Mombasa.[Photo/the-star.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke mmoja ameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa kwa kosa la kumchapa kwa kutumia kiatu mtoto wake mwenye umri mdogo.

Mnamo Disemba 16 mwaka huu katika eneo la Ujamaa eneo bunge la Likoni, Anastacia Matoo anadaiwa kumchapa mwanawe mwenye umri wa miaka 10 kwa kutumia kiatu tukio ambalo lilisababisha kudhohofisha afya yake.

Mtoto huyo alinusuriwa na msamaria mwema baada ya kutoroka na baadae kupelekwa kwenye kituo cha afya.

Mshukiwa alikiri mashtaka dhidi yake na kusema kwamba alikuwa mwenye hasira wakati wa kumuadhibu mtoto huyo.

“Ilkuwa ni hasira ndio nkamuadhibu mtoto hivyo,naomba msamaha”,alisema Matoo.

Kesi yake itasikilizwa  Januari nane Mwakani.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published.* https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF