Mama mmoja na mwanawe wanauguza majeraha katika hospitali ya Embu level five baada ya kupata ajali katika eneo la Kanyonyoo, barabara kuu ya Thika kwenda Garissa.
Akidhibitisha ajali hii chifu wa kata ya Kivaa Josphat Mutiso alidokezea kuwa wawili hao walikuwa kwa pikipiki kabla ya kugongwa kutoka upande wa nyuma na lori moja lililokuwa limepoteza mwelekeo.
Chifu Mutiso alisema kuwa dereva wa lori hili ambaye hakuumia katika ajali hio alikuwa ameshindwa kulidhibiti pale liligonga pikipiki hiyo na kuwaumiza waliokuwemo.
"Mwenye pikipiki hio alikuwa amebeba mamake wakielekea katika shughuli zao kabla ya kugongwa na lori moja kutoka upande wa nyuma," alisema Mutiso.
Wawili hawa waliopata majeraha ya kichwa na miguu walikimbizwa katika hospitali ya Kivaa health centre kwa huduma ya kwanza kabla ya kuhamishwa na kupelekwa hospitali kuu ya Embu kwa matibabu zaidi.