Wanafunzi 23 walionusurika kifo  katika shambulizi la Garissa kutoka kaunti ya Nyamira  wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea usaidizi kutoka kwa mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Alice Nyachoka Chae.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza afisini mwake katika kaunti ya Nyamira mnamo siku ya Jumapili mwakilishi  huyo alisema aliamua kuwapa usaidizi wa nguo wanafunzi hao 23  walionusurika kifo katika chuo cha Garissa ili kurejelea masoma yao bila taswishi yoyote.

Wakati uo huo , mwakilishi huyo alisema wanafunzi hao wanastahili kusaidiwa zaidi maana wallipoteza nguo zao na hata pesa huku wakiendelea kujiandaa kurudi shuleni katika chuo kikuu cha Moi kilichoko Eldoret kaunti ya uasinigishu.

“Wanafunzi hawa ndio watatusaidia kesho baada ya kusoma masomo ni jambo nzuri zaidi katika Jamii hawa ndio viongonzi wa kesho na wanastahili kusaidiwa zaidi ili waendelee na masomo yao,”alisema Alice Chae mwakilishi wa wanawake kaunti ya Nyamira.

Aidha,  wanafunzi hao walionekana kuwa na furaha baada ya kukumbukwa na kiongonzi huyo alipowakabidhi nguo mwakilishi huyo.

“Kwa upande wangu namshukuru kiongonzi wetu Alice kwa kutusaidia nguo maana tulipoteza kila kitu na tumekuwa tumeshindwa cha kufanya mungu ambariki,”alihoji Betty Moraa mwanafunzi aliyenusurika Garissa.

Viongonzi wote wameombwa kuwa na moyo wa kuwasaidia wanafunzi kama hao wanapokuwa katika hali ngumu ili kuendelea na masoma pamoja na maisha yao hayo ni kwa mijibu wa mwakilishi huyo.