Muungano wa upinzani wa Cord unastahili kujiunga pamoja na kuunda chama kipya iwapo wanahitaji kujiimarisha kisiasa.
Chama cha ODM ambacho ni chama ambacho kiko na umaarufu katika muungano huo, kimekuwa katika siasa kwa zaidi ya miaka kumi, huku vyama ambavyo huundwa upya vikiendelea kujiimarisha na kuunda serikali nchini.
Ikumbukwe kuwa Chama cha NARC kilichobumiwa hapo mbeleni kilishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002, kupitia Rais mstaafu Mwai Kibaki.
Ilipofika mwaka wa 2007, Rais Kibaki aliunda chama kingine cha PNU na kupata ushindi kwa mara ya pili.
Ilipofika mwaka wa 2013, Rais Uhuru Kenyatta aliwania uongozi kupitia chama kipya cha TNA, na kupata ushindi kupitia ushirikiano wa chama kipya cha URP.
Hili linaashiria kuwa uongozi unaendelea kubuniwa kupitia vyama vipya kila kuchao.
Muungano wa Cord unastahili kuvunja chama cha ODM ambacho kimeoneka kukumbwa na mengi katika siku za hivi karibuni, na kuunda chama kipya,
Aidha, vyama vya Wiper na Ford Kenya vinafaa kuendelea kuungana katika muungano huo wa Cord, na kuunda chama kipya cha kisiasa.
Wakichukua hatua hiyo, Raila Odinga, Kalonzo Muzyoka na Moses Wetangula, watakuwa katika hali ya kupambana na Jubilee katika kupata ushindi wa 2017.