Licha ya serikali kuu pamoja na zile za kaunti kupitia Wizara za Afya kubuni njia mbalimbali za kuwasaidi wanawake wajawazito wakati wa kujifungua kwa kujenga vituo ama zahanati mbalimbali kote nchini ili kuafikia malengo ya mwaka wa 2030, visa vya kina mama kufariki wakati wa kujifungua bado vinashuhudiwa nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kisa cha hivi majuzi kikiwa katika eneo la Pwani ambapo mama mmoja aliripotiwa kufariki katika hospitali moja ya serikali.

Idaiwa kuwa mwanamke huyo, ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kujifungua, alifariki katika zahanati moja huko Ganze baada ya kukosa huduma za dharura alipokuwa akijifungua.

Mama huyo aliyekuwa anahitaji kufanyiwa huduma za kwanza kabla ya kusafirishwa hadi katika Hospitali Kuu ya Kilifi ili kufanyiwa uchunguzi inaarifiwa alifariki bila hata kuhudumiwa na mhudumu yeyote wa afya katika zahanati hiyo.

Tukio hilo lilipelekea mwakilishi wa wadi katika eneo hilo Emmanuel Chai kuwaandikia wakuu wa wizara ya afya katika hospitali hiyo kuwataka kuanzisha uchunguzi mara moja ili kubaini iwapo kulikuwa na utepetevu miongoni mwa wahudumu wa afya waliokuwa kwenye zamu.

Kisa hicho kiligadhabisha viongozi wa serikali kwa vile mama wa taifa Magret Kenyatta alianzisha kampeni ya Beyond Zero ili kuona kwamba idadi ya kina mama wajawazito wanaoaga dunia inapungua hadi asilimia sufuri kote nchini.

Bi Kenyatta alitenga vituo vya beyond zero kote nchini ili kina mama waweze kujua hali zao afya na hata kusaidiwa ili kujifungua bila kutatizika.

Kwa sasa swali lililosalia miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo ni iwapo uchunguzi unaofanywa utawatambua wahudumu wa afya waliokuwa kwenye majukumu au la, na iwapo watajulikana, watachukuiliwa hatua gani kisheria?