Ajali iliyotokea hivi majuzi katika kivuko cha feri ya Likoni imeonesha mwanya uliopo katika kitengo cha kukabili mikasa ya dharura katika kivukio hicho.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Tukio hilo lilifanyika siku chache baada ya makadirio ya bajeti ya taiafa kudhibitisha ununuzi wa feri mbili zitakazopunguza msongamano unaoshuhudiwa katika kivukio hicho.

Mradi huo utagharimu nusu bilioni, ushuru uliotozwa mwananchi wa kawaida.

Miongoni mwa walipaushuru hao ni mwendazake Joel Masindano, aliyefariki baada ya gari alilokuwa akiendesha kutumbukia katika kivukio hicho.

Tukio hilo lilidhihirisha wazi pengo linalostahili kushughulikiwa haraka, ili kuwezesha shirika la huduma za feri nchini kutoa huduma za dharura katika wakati mwafaka.

Kwa zaidi ya siku mbili, shirika hilo pamoja na polisi walikosa kufanikiwa kutoa gari aina ya Probox lililohusika katika ajali hio.

Iliwalazimu wapiga mbizi kutoka halamashauri ya forodha kusaidia katika oparesheni hio na kutoa gari hilo lililokuwa futi 60 ndani ya bahari.

Mwenyekiti wa shirika la wapiga mbizi na waokoaji nchini Bw Owaga alidai kuwa shirika hilo halijaajiri kitengo maalum cha kukabili mikasa, licha ya kuwa ni miaka zaidi ya ishirini sasa tangu mkasa wa feri ya Mtongwe kutokea mwaka 1994.

Kivukio hicho cha feri kinaripotiwa kutumiwa na takribani watu 300, 000 na magari 6, 000 kwa siku.

Baada ya mkasa wa Mtongwe kutokea, jopo maalum likiongozwa na Mbogholi Msagha liliundwa ili kuweka mikakati ya kukabiliana na majanga ya dharura lakini miongo miwili baadae, bado suluhu haijapatikana.

Shirika la huduma za feri linahitaji kitengo maalum kitakachoweza kuokoa maisha na mali ya wakaazi katika kivukio cha Likoni wakati wa mikasa, kwani wananchi wanaotumia kivuko hicho wanalipa ushuru kama mwananchi yeyote yule.