Swala la misongamano mijini limekidhiri kwa kiasi kikubwa, huku magari, watu na hata mifugo waking’ng’ania nafasi ya katika miji yetu. Hata hivyo, swala la misongamano ya magari ndilo sugu zaidi, huku kila mtu akitaka hatua mwafaka zichukuliwe ili kudhibiti ongezeko hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mojawapo ya sababu ni kutokuweko kwa njia mbadala za kuwawezesha wasafiri na wenye magari wanao pitia mijini pasi na shughuli makhususi. Magari mengi yanayotoka viungani, miji hadi miji, mikoa hadi mingine nakadhalika yanajipata mijini. Barabara pana zote zinaelekezwa kwenye barabara nyembamba za mijini na majijini hasa jiji la Nairobi.

Misongamano hii imezua changamoto si haba katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano. Wagonjwa mahututi wengi wamefia barabarani kwa kutofikishwa mahospitalini kwa dharura. Kina mama wajawazito pia wametatizika kuhudumiwa hospitalini na zahanatini kutokana na tatizo lili hili. Wazima moto nao hawajasita kukabiliana na ghadhabu ya wananchi baada ya kuwasili penye mikasa wakiwa wamechelewa.

Vyuo vikuu vingi vimesababisha kuwepo kwa magari meengi yanayoletwa na kupitia mijini. Wakati wa mahafala (graduation), wasimamizi wa vyuo wanafaa kupewa mbinu mbadala za kuelekeza magari na maegesho yake kuzuia misongamano huu.

Sekta ya uchukuzi ina jukumu la kusaidia kuwaleta washikadau wote kuibua mbinu za kupunguza swala hili lote la misongamano. Hili likishughulikiwa vizuri, huduma ya usafiri itatekelezwa kwa uafaka.