Watoto wengi mitaani hawana uelekezi mwafaka kuhusu namna ya kutumia wakati wao wa ziada barabara. Nyakati za shuleni ni rahisi kwa walimu kwa ushirikiano na wazazi kuwawelekeza. Klia mara walimu huwapa kazi za ziada za mafunzo, huku nao wazazi hutwikwa wajibu wa kutia sahihi kwenye shajara kama ishara kwamba kazi hiyo imefanywa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Sasa ni muhali kuwapata watoto vitabuni, kisa na maana; ati ni likizo na kazi nyingi ya ziada ilimalizika. Kwa sasa watoto wako kwenye runinga na redioni kutazama na kusikiliza vipindi wanavyo vienzi kama vile vibonzo(cartoon), ambavyo vinawazuzua wengi kubaki kuzubaa tu na hata kusahau kazi walizo twaliwa. Wazazi hawana uthabiti kwa kuwa wameambukizwa maradhi ya TB (Too Busy) na kila  uchao na uchwao wamo kwenye tafutatafuta kwa kuweza kukidhi mahitaji ya kimsingi.

Wajibu walio nao wazazi kwa sasa ni kuratibu mipango ya kuwawezesha watoto wao wasijihusishe kwenye tabia mbi na zisizostahiki. Watoto wapewe uelekezi wa ratiba ya masomo ili wasome wakiwa nyumbani, na pia wapewe nafasi ya kupumzika na kujivinjari. Fursa hii pia ni murwa kwa wasichana kwa wavulana kufunzwa kazi za nyumbani kama vile kufua, kupika na hata kuwaosha watoto.

Maswala ya kushona ni muhimu kwa watoto hasa kuziba mianya kwenye nguo zao na ata pamoja na . Haya pamoja na ukarabati wa vifaa vya nyumbani. Itakuwa ajabu ya kama kumwona binadamu akienda mbinguni kwa baiskeli kuona wanafunzi wengi hawajui vifaa vya ufundi na hata matumizi yake. Watoto wengi hutembezwa maeneo ya mashambani kwa dhamira hii, na yote haya yatachangia kumkuza mtoto kwa malezi mwafaka ili awe wa kuwajibika na wa kujitegemea.