Wanafunzi shuleni wanafunzwa masomo mengi yakiwa na dhamira ya kuwawezesha wanafunzi kuwa wenye uwezo wa kuingiliana kijamii. Wanafunzi wawe wenye kujitafutia ajira za kibinafsi. Serikali imejizatiti ilikuwezesha watoto kukubalika katika jamii pasipo mtaguzano hasi. wanafunzi wanafunzwa Kiingereza, Kiswahili, Sayanzi, Hisabati na Somo la Elimu jamii na Dini.
Kuna masomo mengi yaliyoondolewa na kutemwa kwenye msururo huo; somo la kilimo lilikuwa lenye manufaa kwa wengi. Watoto waliweza kujihusisha na shughuli za ukulima, hasa baada ya mtihani wa darasa la nane. Wengi waliweza kukuza mboga na mimea mingine. Aidha Mifugo kama sungura, mbuzi, kuku na ndege wakufugwa walihusishwa. Kupitia haya, wazazi walisaidiwa ili kuandaa vifaa kwa minajili ya kujiunga na shule za upili.
Masomo kimu (home science), sanaa (art and craft) na Muziki yalifaa kukuza vipaji ainati kwa watoto. Wanafunzi wa sasa wanahitaji haya masomo kama mbinu mbadala wakuendeleza tajriba zao na hata talanta. Visa vya ukosefu wa ajira, hasa katika wilaya ya Kiambu unaweza suluhishwa na haya.
Shule nyingi zimezindua mbinu za kilimo ili kuwapa chakula na kujinufaisha na mbinu za kilimo pamoja na ukuzaji wa mimea na mifugo. Walimu wakuu wameshikana kuwasaidia mayatima na wasioweza kwa lisho. Walimu wakuu walishirikiana kuwezesha watoto wote kusoma pasi na tumbo tupu.
Kwa ushirikiano, walimu waasiwe kushikana kuwasaidia wanafunzi waelimike na wawe na lishe bora shuleni.