Wagonjwa wakiwa wamelazwa hospitalini. [Picha/the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa changamwe wanahofia kuzuka kwa maradhi hatari ya ya onyang’nyong’ ambayo yanahataraisha maisha ya wakazi wengi eneo hilo.

Wakizunguumza na meza yetu ya habari wakaazi hao wameeleza kushangazwa na mkurupuko wa maradhi hayo ambayo tiba yake bado haijatambulika, wakisema yanadalili za kupoozesha viungo vya mwili.

Wanataka hatua za dharura zichukuliwe ili kudhibiti maradhi ya onyang’nyong’ ambayo yanahataraisha maisha ya wakazi wengi eneo hilo.

Nao wahudumu wa boda boda boda,wakiongozwa na Salim Juma,wanasema  visa vya kuwabeba wagonjwa eneo hilo kuwapeleka hospitalini vimekuwa vya kuogofya kwani wanahofia kuambukizwa wakiwa kazini.

“Tunahofia kuwabeba abiria wanaouguwa ugonjwa huo,wanaweza kutuambukiza”,alisema Juma.

Ugonjwa huu umetajwa kusababishwa na mbu wa mchana wengi wakimtaja mbu huyo kuwa wa rangi ya kijani na ambaye anaweza hata kumlemaza binadamu pale hatua za dharura zinapokosa kuchukuliwa.

Licha ya wakazi wa  Changamwe kulalamikia kuweko na mkurupuko wa maradhi ya onyang’nyong’ wizara ya afya imesema kuwa haijathibithisha kuweko na maradhi hayo kwa sasa katikati kaunti ya Mombasa kwa jumla.

Akizungumza na mwanahabri huyu siku ya Ijumaa, afisa wa mawasiliano ya kaunti ya Mombasa Richad Chacha, alisema kuwa idara hiyo kupitia kwa mkurugenzi wake mkuu Khadija Shekel wamefanya uchunguzi kuhusiana na madai ya maradhi hayo lakini hawajabaini kuwepo kwa maradhi hayo.

Hata hivyo amethibisha kuwepo kwa maradhi ya chikungunya ambapo kati ya visa 120 vilivyofanyiwa uchunguzi visa 32 vimethibithishwa kuwa na virusi hivyo vya chikungunya.

Aidha wakaazi wametakiwa kuchukua tahadhari na kuyaeka mazingira yao masafi huku serikali ya kaunti ikizidisha mikakati yake ya kukabiliana na magonjwa hayo kwa kuhakikisha kuwa mazingira yote yalio na maji yaliozagaa yakitibiwa ili kumaliza makaazi ya mbu wanasababisha maradhi hayo.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published. https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF