Jaji mkuu David Maraga. [Osman Suleiman]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Jaji mkuu David Maraga ameitaka serikali kutenga fedha za kutosha kwa idara ya mahakama ncini ili iweze kufanikisha miradi ya ujenzi wa mahakama mbali mbali nchini.

Maraga amesema majengo mengi ya mahakama yamesimama kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha kwani kiasi cha fedha kinachopewa kwa idara hiyo kinatosheleza mishahara ya wafanyikazi na huduma nyengine ndogo ndogo.

Akizungumza siku ya Jumatatu wakati wa uzinduzi  rasmi wa jengo la mahakama kuu kaunti ya Kwake, Maraga alisema kuwa iwapo idara ya mahakama itatengewe fedha za kutosha kuna uwezekano wa kuboresha huduma zaidi katika mahakama mbali mbali nchini, ili wananchi wapate kuhudumiwa ipasavyo.

Maraga amelalamikia vitisho vya kila mara kutoka kwa wanasiasa dhidi ya idara ya mahakama akisema vinaathiri utendakazi wao. 

Maraga anasema vitisho hasa kuhusiana na kupunguzwa bajeti ya idara hiyo kwa sababu ya baadhi ya maamuzi yasiowapendeza wanasiasa yamechangia miradi kadhaa kukwama.

 Maraga amewalamu wabunge kwa kutishia kupunguza kiwango cha fedha za idara ya mahakama kila wanapokwaruzana na idara ya mahakama hasa katika kesi ambazo serikali upoteza.

Alisema kuwa mahakama kuu ya Kwale itagharimu shilingi milioni 390.

Aidha amewaonya maafisa wa idara hiyo wanaotumia mali ya umma visivyo au kujihusisha kwenye ufisadi kwamba watakabiliwa vilivyo.