Jaji mkuu nchini David Maraga katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Idara ya mahakama nchini imesema kwamba haitaruhusu kesi za ubakaji hasa zinazohusu watoto kusikilizwa nje ya mahakama.

Jaji mkuu nchini David Maraga amesema kuwa watu wengi wamekua na mtindo wa kusuluhisha kesi hizo nje ya mahakama, hatua aliyosema imepelekea watoto wengi kunyimwa haki zao za kimsingi.Maraga alisema ni jambo la kusikitisha kuona wabakaji wakiachiliwa huru bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, Maraga alisema kuwa watakabaliana na watu ambao hujitokeza kuwatishia watoto ili wasitoe ushahidi, kama njia moja ya kuhakikisha kesi hizo zinasikizwa na kuamuliwa bila pingamizi yeyote, ili watoto wapate haki.

Maraga vile vile amesema kuwa kesi za watoto zitapewa kipau mbele punde zinapowasilishwa mahakamani, kuhakiisha zinaamuliwa kwa haraka ili kuepuka hali ya watoto kusahau ushahidi.