Jaji mkuu nchini David Maranga amesema kuwa heunda kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi zikaongezeka mwaka ujao, ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2013.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza kwa niaba ya Maraga wakati wa sherehe za kustaafu kwa majaji Anyara Emkhule na John Mwera huko Mombasa, naibu jaji mkuu nchini Philemona Mwilu alisema hali hiyo huenda ikashuhudiwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya Wakenya wanaounga mkono wagombea tofauti huku idadi ya wawaniaji wa viti tofauti pia ikiongezeka.

Maranga alisema katika uchaguzi wa mwaka 2013, kesi 188 zilisikizwa na kuamuliwa kote nchini.

Alisema kuwa atahakikisha kesi hizo zinasikizwa haraka bila kuahirishwa, ili zikamilike kwa wakati unaofaa na wahusika kuchukuliwa hatua kali, iwapo watapatikana na hatia.