Serikali ya Marekani kupitia Balozi wake humu nchini Robert Godec imesema kwamba itasaidia Kenya kupigana na ugaidi.
Balozi Godec amesema kwamba kuna haja ya idara ya usalama humu nchini kuhakikisha kwamba kuna ushirikiano kwa kila mmoja katika vita dhidi ya ugaidi.
Akihutubia kongamano la Magavana mjini Kisumu, Balozi huyo ameongezea kuwa ushirikiano bora baina ya wanasiasa, viongozi wa kidini na waumini unahitajika hasa wakati wa shida.
Alisema ikiwa hayo yote yatazingatiwa, basi itasaidia katika vita dhidi ya itigadi kali za kigeni.
Wakati uo huo, Balozi huyo alisema kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Kenya katika vita dhidi ya ugaidi na uuongozi wa kidemokrasia.
Balozi Godec ameyasema haya wakati ambapo Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa kuzuru Kenya mnano Julai mwaka huu.
Magavana wanakongamana Kisumu ili kujadili mafanikio ya Serikali za ugatuzi miaka miwili tangu ziingie mamlakani.
Kongamano hilo limeingia siku yake ya pili hii leo baada ya kufunguliwa rasmi hapo jana na Rais Uhuru Kenyatta.