Tume huru ya uchaguzi na mipaka ni tume iliyo huru na haifai kuingiliwa na mrengo wowote wa kisiasa katika utendakazi wake.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbali na kufanya kazi yake kwa haki na usawa, IEBC pia inafaa kufanya kazi hiyo kwa njia huru. Shinikizo za hivi punde kutoka upinzani kutaka tume hiyo ifanyiwe marekebisho kunainyima uhuru.

Kuna njia mbadala ya kuhakikisha kuwa tume hiyo imefanya na kutekeleza kazi yake kwa usawa mbali na kusurutisha ifanyiwe marekebisho.

Shinikizo hizo zinadhihirisha tu woga wa upinzani kuwa huenda wakashindwa tena kwa uchaguzi ujao.

Kwa kufanyia tume hiyo marekebisho, ina maana kuea upinzani unataka kuwe na kiongozi mwenye mtazamo wa upinzani na hivyo kutatiza uhuru wa tume hiyo.

Ikiwa kiongozi atachaguliwa kusimamia tume hiyo leo hii, hawezi kuambatana na mikakati iliyopo kuhakikisha uchaguzi wa uwazi umefanyika.

Ikiwa jambo hili lilikuwa mwafaka, lingefanywa mapema kabla hata ya shughuli ya kuandikisha wapiga kura.

IEBC inaweza kusimamia uchaguzi ujao kwa uwazi chini ya msimamizi wa sasa, Isack Hassan.

Upinzani unafaa keteua wakaguzi ambao watashirikiana na wale wa mashirika ya kitaifa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unaendeshwa kwa njia ya uwazi.

Uamuzi huu wa upinzani huenda hata ukazua ghasia iwapo hautasitishwa.