Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Bi Martha Karua amewakashifu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika maandamano ya muungano wa Cord dhidi ya Tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bi Karua amekosoa idara ya polisi kufuatia jinsi walivyokabiliana na waandamanaji wa Cord waliokuwa wakishinikiza kubanduliwa kwa Tume ya IEBC siku ya Jumatatu.

Aidha, kiongozi huyo wa kisiasa amemtaka Waziri wa usalama wa ndani Bwana Joseph Nkaissery kung'atuka mamlakani.

"Visa vya polisi kutumia nguvu kupita kiasi havikubaliki kamwe. Ni haki ya kikatiba ya wananchi kuandamana nchini humu,” alisema Bi Karua.

Alipoulizwa kama atajitokeza kwa maandamano,ya Jumatatu ijaayo, aliliacha jibu wazi.

"Hata kama hamnioni kwa maandamano hayo, hilo halimaanishi kuwa siungi mkono kubanduliwa kwa makamishna wa IEBC kutoka mamlakani,” alisema Bi Karua.