Maafisa wa trafiki katika ukanda wa Pwani wametakiwa kujitahidi ili kuhakikisha hakuna msongamano wa magari kuanzia eneo la Mazera hadi katikati mwa jiji la Mombasa.
Akizungumza afisini mwake siku ya Jumatano, mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa, amesema kuwa msongamano huo unasababishwa na maafisa wa trafiki wasiowajibika.
Marwa amemtaka mkuu wa trafiki ukanda wa Pwani Emmanuel Okanda na mwenzake wa kaunti Nahid Musa kuhakikisha wanashirikiana kutatiza tatizo hilo.
Marwa alisema kuwa msongamano huo unatatiza watalii, hasa kwa kuwachelewesha kufika kwa wakati ufao.
Aidha, amewataka maafisa hao kushirikiana na wale wa kaunti yaani kuhakikisha tatizo la misongamano ya magari haishuhudiwi tena.