Mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa amesema kuwa idara ya usalama imeweka mikakati thabiti ya kuimarisha usalama msimu huu wa kampeni na hata wakati wa uchaguzi mkuu.
Marwa alisema wamechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa maeneo ya Pwani yamekuwa yakishuhudia viongozi wa kisiasa wakivuruga amani wakati wa kampeni na uchaguzi.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi yake siku ya Jumatano, Marwa alidokeza kwamba idara ya usalama iko macho kukabiliana na watu watakao kuwa na nia ya kuvuruga amani wakati wa uchaguzi.
Amewataka wakuu wa idara ya uslama katika kaunti zote sita za Pwani kuwatia nguvuni wanasiasa watakao wachochea wakaazi kuzua vurugu.
Wakati huo huo, Marwa amewataka vijana kujitenga na viongozi wa kisiasa wenye nia ya kuwatumia kwa maslahi yao ya kibinafsi.