Mshirikishi wa eneo la Pwani Nelson Marwa amefichua maeneo yanayohusika katika uingizaji wa bidhaa gushi nchini.
Marwa alisema bidha nyingi za magendo kutoka Pemba na Zanzibar hupitia bandari ya Shimoni pasi kufuata sheria.
“Kuna bidhaa nyingi za magendo zinazopitishwa kupitia eneo la Shimoni,” alisema Marwa.
Alisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wanaojihusisha katika biashara ya magendo eneo zima la Pwani.
“Tutahakikisha biashara ya magendo inasitishwa eneo la Pwani,” alisema.
Marwa amewataka polisi kufanya msako mkali dhidi ya biashara hizo za magendo katika eneo nzima la Pwani.
Ikumbukwe bidhaa zenye thamani ya mabilioni ya pesa zilichomwa eneo la Pwani baada ya kugundulika kuwa zilikuwa za magendo mapema mwaka huu.