Mshirikishi wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Picha/ nation.co.ke]
Mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa ametilia shaka utendakazi wa Mahakama ya Mombasa.
Marwa amedai kuwa mahakama hiyo inatumika kukandamiza haki za Wakenya.Alidai kuwa mahakama hiyo inatumiwa vibaya na serikali ya kaunti ya Mombasa kuwahangaisha wakaazi wasiokuwa na hatia hasa wahudumu wa matatu.“Maaskari wa serikali ya Mombasa wanatumia mahakama hii kuwakandamiza Wakenya pasi makosa yoyote,” alisema Marwa.Marwa alisema kuwa amepokea malalamishi mengi kutoka kwa wakaazi wanaoshtakiwa katika mahakama hiyo pasi sababu zozote.“Wananchi wanalalamika sana kuhusu jinsi mahakama hiyo inavyoendeleza shughuli zake,” alisema Marwa.Marwa wakati huo huo alitoa onyo kwa maafisa wa polisi wanaotumiwa vibaya na wanasiasa.Kauli hii inajiri baada ya kaunti ya Mombasa kumshtaki mwaniaji wa ugavana Hezron Awiti kufuatia kuweka mabango ya kisiasa mjini humo.Wapinzani wa Gavana Joho wamekuwa wakilalamika kuhusu kunyimwa nafasi ya kuweka mabango yao.