Mshirikishi mkuu wa usalama katika ukanda wa Pwani Nelson Marwa amezionya serikali za kaunti dhidi ya kujisifia kutokana na miradi ya serikali kuu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Marwa aliwaonya wanasiasa dhidi ya kuwahadaa wakaazi kuwa miradi hiyo imetekelezwa na serikali za kaunti.

Marwa amesema kuwa katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na tabia ya baadhi ya serikali za kaunti kudai kutekeleza miradi fulani katika maeneo yao, ilhali serikali ya kitaifa ndio hufadhili wakuu wa miradi hiyo.

Marwa alisema hali hii inaleta mkanganyiko miongoni mwa Wakenya, wasijue miradi gani ni ya serikali kuu na gani ni ya serikali za kaunti.

“Katika siku za hivi karibuni, tumeona serikali za kaunti zikibandika vibao katika miradi ya serikali ya kitaifa na kudai kuwa kaunti ndio imetekeleza miradi hiyo. Hiyo ni kudanganya Wakenya,” alisema Marwa.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Mbunge wa Kilifi Kaskazini Gedion Mungar’o aliyekiri kuwepo kwa tabia hiyo inayoendelezwa na baadhi ya magavana.