Mshirikishi wa usalama katika ukanda wa Pwani Nelson Marwa amesema kuwa atawasilsha pendekezo kwa serikali kuu ili viongozi wanosimamia mpango wa Nyumba Kumi walipwe mshahara.
Akihutubia baraza la usalama katika eneo bunge la Mvita siku ya Jumanne, Marwa alisema kuwa ni bora serikali iwajali watu wanaolinda usalama katika vitengo vyote.
“Nitazungumza na idara ya usalama na kumuandikia Rais Uhuru Kenyatta barua kuhusu swala hili,” alisema Marwa.
Viongozi wa mpango wa Nyumba Kumi wamekuwa wakitoa huduma zao kwa serikali haswa kwa wakuu wa idara ya usalama katika kaunti bila malipo yoyote.