Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Idara ya polisi inasema kuwa imegundua ujanja unaotumiwa na walanguzi wa silaha katika kaunti ya Mombasa.

Akiongea na wanahabari siku ya Jumatatu mjini humo, kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa alisema walanguzi hao wanaoaminika kuleta silaha hizo kupitia kaunti ya Lamu huziweka ndani ya mizigo mingine ili kukwepa kunaswa na polisi barabarani.

“Mtu anabeba mzigo leseni inaonyesha kuwa ni samaki kutoka Lamu, anaweka silaha chini alafu samaki anaweka juu, serikali iko macho,” Marwa alieleza.

Hata hivyo, kamishna Marwa anasema wamegundua  wahusika wawili wakuu ambao ni wafanyabiashara wanaohusika na ulanguzi huo wa silaha kutoka Lamu hadi Mombasa.

Silaha hizo zinaaminika kutumiwa na genge la vijana katika mitaa ya Majengo na Old Town kwa kuwaangaisha wananchi, na Marwa amewaagiza maafisa wa trafiki pamoja na makamanda wa polisi kuwa makini barabarani.