Idara ya Usalama katika eneo la Pwani imetakiwa kuanza harakati za kuyachunguza magari yenye nambari za usajili za kigeni yanayohusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Alhamisi katika eneo la Diani, Kaunti ya Lamu, Mshirikishi mkuu wa usalama kanda ya Pwani, Nelson Marwa, alisema kuwa magari aina ya Probox yaliyo na nambari za usajili za taifa la Tanzania yanafaa kuchunguzwa kubaini biashara yanayoendesha katika eneo la Pwani.

Aidha, Marwa alisema wakati umefika kwa suala la utumizi wa dawa za kulevya kutangazwa kuwa janga katika eneo la Pwani, kufuatia kukithiri kwa tabia hiyo.

Afisa huyo wa usalama alisema kuwa vijana wengi sasa wanaotumia mihadarati ndio wanaojihusisha katika mambo ya uhalifu na kuwahangaisha wakaazi.