Mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa ametoa hakikisho la usalama kwa wanahabari katika eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na wanahabari walipofika kwenye afisi zake baada ya kushiriki maandamano ya amani kupinga unyanyasaji na dhulma wanazozipata wakiwa nyanjani, Marwa alisema vyombo vya habari vinapaswa kulindwa vilivyo.

Marwa alisema kuwa afisi yake iko tayari kutoa usalama wa kutosha kwa waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa idara ya usalama imeanzisha uchunguzi wa kubaini chanzo cha kifo cha wanahabari waliofariki katika hali ya kutatanisha.

Aidha, alisema kuwa ataanzisha uchunguzi kuhusu mwanablogi anayedai kupata vitisho vyo kuuawa kutokana na kutoa taaarifa kuhusiana na vifo vya wanahabari wenzake.

Akiandamana na maafisa wenzake kutoka idara ya usalama, Marwa alisema vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kufahamisha umma yanayotukia, na hali ya wanahabari kufariki katika hali ya kutatanisha ni jambo la kusikitisha na kukera.

Alisisitiza kuwa afisi yake haitavumilia vitendo kama hivyo.

Maandamano hayo yanajiri baada ya wanahabari jiji Nairobi kushiriki maandamano kupinga swala lilo hilo la mauaji ya kiholela baina yao.