Mratibu mkuu wa ukanda wa Pwani.[barakafm.org]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mratibu wa ukanda wa Pwani Nelson Marwa ametupilia mbali madai kuwa maafisa wa usalama walitoka na kijifucha wakati wa uvamizi uliofanywa na wanamgambo wa Alshabab huko Lamu.

Wiki iliyopita washukiwa wa Al-Shabaab walivamia maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza mabasi ya abiria na kituo cha polisi cha Ishakani ambapo kulizuka madai kuwa maafisa wa polisi walitoroka katika uvamizi huo.

Akizungumza na wanahabari siku ya Ijumaa katika afisi yake, Marwa alisema kuwa maafisa wa usalama walikuwa macho na kukabiliana na wanamgambo hao kulingana na kanuni za idara ya polisi.

Amewapongeza maafisa hao kwa kujizatiti katika kukabiliana na wanamgambo hao na kusisitiza wanafaa kutuzwa.

Alisema hali ya usalama katika ukanda wa Pwani imeimarika na maafisa wa polisi watahakikisha hali hiyo inadumishwa.

Marwa amesema kuwa maeneo yatakayopewa kipao mbele zaidi kwa kuimarisha usalama ni maeneo ya umma hususan katika kivuko cha Likoni na kile cha Mtongwe pamoja na taasisi za elimu ya juu ambayo ni ulengwa na Alshabab.