Haniya Saggar akiwa mahakamani hapo awali. [Photo/ saraarmedia.com]
Kesi ya ugaidi inayomkabili mke wa marehemu Sheikh Aboud Rogo itasikilizwa leo, September 4, 2017 katika Mahakama ya Shanzu.
Haniya Said Saggar, alitiwa mbaroni mwaka jana, akiwa nyumbani kwake huko Kanamai, Kaunti ya Kilifi.Jumla ya mashahidi watano tayari wametoa ushahidi wao, huku mashahidi wawili wakitarajiwa kufika mbele ya mahakama kesi hiyo itakaporejelewa.Saggar pamoja na wasichana wengine wanne wanadaiwa kuhusika na magaidi walioshambulia Kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa mwaka jana.Kenya inaendelea kukabiliana na ugaidi tangu mwaka 2012, ilipotuma wanajeshi wake nchini Somalia kukabiliana na wanamgambo wa al-Shabaab.