Mashahidi watatu wamesusia kesi ya ubakaji ya msichana wa darasa la tano mwenye ujauzito, licha ya wao kufahamishwa kuhusu kikao cha kesi hiyo.
Mashahidi hao hawakutoa sababu zozote za kukosa kuhudhuria kikao hicho, hata baada ya wao kujulishwa mapema.
Hatua hiyo imemlazimu Hakimu Henry Nyakweba kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 15, mwaka huu.
Nyakweba ameitaja hatua ya kukosekana kwa mashahidi hao kama inayolemaza juhudi za mahakama kusikiliza kesi hiyo kwa haraka.
“Kwa vile hakuna mashahidi, basi sina budi ila kuahirisha kesi hii,” alisema Nyakweba.
Kesi hiyo inamkabili Said Hamisi anayedaiwa kumbaka mtoto huyo mnamo April mwaka huu katika eneo la Likoni.