Katika juhudi za kukabiliana na maswala ya itikadi kali na uhalifu katika kaunti ya Mombasa, sasa mchakato wa kijamii ya kuunda sera itakayofanikisha jitihada hizo wazinduliwa rasmi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini Haki Afrika limechukua hatua ya kukusanya maoni kutoka kwa jamii ili kuunda sera maalum itakayowaongoza watetezi hao wa haki za kibinadamu, Serikali kuu na ile ya Kaunti ya Mombasa.

Katika mkao na Wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid alisema kuwa itikadi kali, ugaidi na uhalifu ni matatizo ya kiusalama na ni lazima jamii ihusishwe katika kuyatatua.

Khalid aliisihi Jamii katika kaunti ya Mombasa kuwasilisha maoni na mapendekezo yao kwa shirika hilo huku viongozi wa kidini na wale wa Serikali wakihimizwa kutoa kauli yao kuhusu jinsi tatizo hilo linaweza kutanzuliwa.

“Tunawaomba wakaazi na jamii kwa jumla kuhakikisha kuwa inawasilisha maoni yao kuhusiana na jinsi tutakavyoweza kukabiliana na maswala ya utikadi kali na uhalifu,” alisema Khalid.

Tayari shirika hilo limethibitisha kujitokeza kwa wanaharakati wa kijamii kutoa maoni yao na kusema kuwa zoezi hilo litachukua takribani wa miezi mitatu.