Afisa wa mipango katika taasisi ya afya na maendeleo barani afrika yaani, African Institute for Health and Development' Hamisi Suleiman Dzole amependekeza mashirika kuwasilisha miradi yao katika serikali ya kaunti ya Mombasa kabla ya kuianzisha miradi hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika kongamano la mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Suleiman amesema kuwa mashirika mengi katika kaunti hiyo yamekuwa yakiendeleza miradi yao bila kuwasilisha katika serikali ya kaunti na hatua hiyo ni kinyume cha sheria.

Ameleza kuwa ni vizuri mashirika yanayojitokeza yaweze kuwasilisha miradi yao katika serikali ya kaunti sambamba na kuwahamasisha wananchi kabla ya kuanzisha ili kuweza kunufaika na kuwanufaisha wakaazi wa kaunti hiyo.

"Tumepokea malalamishi kutoka kwa wakaazi wa kaunti hii kuwa kuna baadha ya mashirika yanaendeleza miradi yao bila manufaa yoyote kwa wananchi na maswala hayo yanafaa kuwanufaisha wananchi ndiposa twasema lazima wajulishe serikali ya kaunti ya Mombasa kabla ya kufanya kiradi hiyo," alisema Dzole.

Hata hivyo, ameyataja mashirika hayo kuwa hayana manufaa kwa wakaazi kwani hawana uthibitisho kamili kutoka kwa serikali.

Picha: Mashirika mbalimbali yasiokuwa ya kiserikali ya kongamana katika mazungumza ya uwekezaji Mombasa. Wamependekeza mashirika kuwasilisha miradi yao katika serikali ya kaunti ya Mombasa kabla ya kuianzisha miradi hiyo.