Mashirika mbalimbali yameombwa kujitokeza kusaidia vijana katika eneo la Pwani kujinasua kutoka janga la mihadarati.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne, mkurugenzi mkuu wa shirika la Reach Out Trust Centre Taib Abdulrahman, alisema vijana wengi wameshindwa kujikimu kimaisha baada ya kupata matibabu, na kuwataka washikadau kutoa msaada kwao kama vile kuwapa ajira.

Abdulrahman pia amewataka wazazi wa waathiriwa wa dawa za kulevya kuchukua jukumu la kuwaangalia na kuwakubali katika jamii, kwa kusema kuwa kazi ya kuwatunza waathiriwa hao sio jukumu la mashirika pekee yake.

Haya yanajiri huku waathiriwa wengi wakilalamika kutengwa na jamii hata baada ya kuchukua hatua ya kujinasua katika mtego huo ambao umekua donda ndugu katika eneo la Pwani.

Wakati huo huo, waathiriwa hao wameiomba serikali kuu hususan Wizara ya Afya kuwasaidia na dawa aina ya Methanol ambayo imekuwa ikiwasaidia na kupelekea wao kusahau dawa za kulevya.

Baadhi ya waathiriwa wamepongeza huduma wanazopewa na shirika hilo na kuapaa kutotumia tena dawa hizo kwa kusema kuwa zimewasababishia matatizo makubwa katika maisha yao.