Mashirika mbalimbali zinataka maafisa ws GSU waliotumia nguvu kupitia kiasi wakati wa maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi mapema Jumatatu wachukuliwe hatua.
Ikiwemo tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu na like la IMLU aidha yanamtaka mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, Keriako Tobiko kuwashtaki maafisa hao kwa kukiuka haki za kibinadamu.
Peter Kiama, mkurugenzi mkuu wa IMLU alisema hakuwa na haja ya vikosi vya usalama kutumia nguvu na kuingia chuoni humo kuwafurusha wanafunzi waliozua rabsha kupinga uchaguzi wa Babu Owino kama mwenyekiti wa muungano wanafunzi SONU.
Maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi yaling'oa nanga punde tu Babu Owino alipotangazwa kuwa mshindi kwa muhula wa nne kama miongozi wa SONU na kumshinda mpinzani wake wa karibu aliyepata kura 3000, huku Babu akiwa na kura 18,000.
Chuo kikuu cha Nairobi kilifungwa baada ya wanafunzi hao kuchoma afisi za SONU na baadaye kuchoma bweni kupinga kuondolewa chuoni humo kwa misingi kuwa walitaka kujiandaa kufanya mtihani uliofaa kung'oa nanga Jumatatu juma lijalo.