Maskwota jijini Mombasa wameunga mkono hatua ya kuvunjiliwa mbali bodi za ardhi kote nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza na mwanahabri huyu siku ya Alhamisi, Hussein Salim mkazi katika shamba la Waitiki eneo la Likoni alisema kuwa hatua hiyo itapunguza mizozo ya ardhi inayowakumba maskwota nchini.

Aidha, aliongeza kuwa itapunguza ufisadi uliokuwa unashuhudiwa kutoka kwa maafisa wa bodi hizo.

Hatua hii inajiri baada ya waziri wa ardhi nchini Jacob Kaimenyi kuvunja bodi zote za ardhi nchini kama njia moja wapo ya kukabiliana na ufisadi, huku akisema bodi hizo zimekuwa zikiendeleza ufisadi nchini.

Aidha, ameongeza kuwa baadhi ya wanachama wa bodi hiyo wamefanya kazi kwa zaidi ya miaka saba, n kuagiza kuundwa kwa bodi mpya za ardhi nchini chini ya kipindi cha wiki mbili.

Bodi hizo zitaongozwa na manaibu makamishina wa kaunti nchini na wanachama wawili kutoka kwa serikali za kaunti.

Bodi hizo zilizovunjwa ziliteuliwa tangu mwaka 2009 na 2012.