Mti wa mipapai ukiwa na matawi yake. [Photo/shutterstock.com]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wizara ya Afya imetoa wito kwa wakaazi wa Mombasa walio na ugonjwa wa Chikungunya kuacha kula matawi ya mipapai kwa imani kuwa matawi hayo yatawaponya ugonjwa huo na kuonya kuwa matawi hayo yanaweza kuwa na madhara kwa figo.

Badala yake wizara ya Afya imewataka wakaazi kutafuta matibabu.

Kufikia sasa visa 32 vimeripotiwa kaunti ya Mombasa huku visa 435 vikiwa bado havijaripotiwa.

Wakati wa kikao cha Afya siku ya Ijumaa, mtaalamu wa magonjwa katika chuo kikuu cha Agha Khan Prof Rodney Adam alisema kuwa ni vigumu sana ugonjwa wa Chikungunya kusababisha vifo lakini husababisha madhara.

Kufikia sasa hakuna vifo vyovyote ambavyo vimeripotiwa huku ugonjwa huo ukiwa umeathiri kaunti zote ndogo sita huku kaunti ndogo ya Mvita ikiripoti visa vingi vikiwa 140.

Kaunti zingine ndogo ni Nyali na visa 20, Kisauni na visa 63, Likoni na visa 104, Jomvu na visa 43 huku kaunti ndogo ya changamwe ikiripoti visa 65.

Tayari serikali ya kaunti ya Mombasa kupitia kwa wizara ya Afya imesema kuwa itakuwa ikikutana kila mara ili kuchunguza hali ilivyo ya uginjwa huo.

Kulingana na shirika la Afya duniani WHO, Chikungunya ni ugonjwa ambao unasambazwa na virusi kutoka kwa Mbu.

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa Chikungunya ni kupatwa na homa nyingi ya ghafla ikiambatana na maumivu ya misuli, kichwa, kichefuchefu, upele na uchovu.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published.* https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF