Kufuatia kauli iliyotolewa na Waziri wa elimu nchini Daktari Fred Matiangi ya kuharamisha likizo fupi za katikati ya mihula sambamba na maombi wakati mitihani ya Kitaifa inapokaribia,limetajwa kutokuwa suluhu la wizi wa mitihani nchini.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baadhi ya Wazazi mjini Mombasa wametoa hisia zao na kupinga pendekezo la Matiangi huku wakisema kwamba tatizo kuu ni Baraza la mitihani nchini KNEC na wala sio Wanafunzi au Wazazi.

Wakizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa na wanahabari huyo, Wazazi hao wamesema kwamba kuharamishwa kwa likizo za katikati ya muhula sambamba na kuharamisha maombi sio wazo mwafaka katika mtaala wa elimu humu nchini.

"Mimi sio kama hatua ya Matiangi itasaidia kusitishwa wizi wa mtihani kwani kuzuia wazazi kuwatembelea watoto wao ama kusitisha kwa likozi za katikati ya muhula hiyo sio suluhisho, la muhimu ni waziri kujadiliana na wadau wa sekta ya elumu na wazazi," alisema mmoja wa wazazi hao Micheal Munyia.

Waziri huyo ametakiwa kuisitisha mbinu hiyo mpya ya kubandua likizo fupi za katikati ya muhula yaani ‘Half-term’ sambamba na maombi kwa Wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya darasa la nane KCPE na kidato cha nne KCSE.