Waziri wa elimu nchini Fred Matiangi amewaonya walimu wakuu wa shule zote katika kaunti ya Kisii dhidi ya kutumia rasilimali za umma kujinufaisha wenyewe.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa baadhi ya walimu hao hutumia rasilimali za umma kushughulikia mahitaji yao binafsi.

Akizungumza mnamo siku ya Jumatano katika shule ya upili ya wavulana ya Kisii katika mkutano wa walimu wakuu wa shule zote za upili katika kaunti ya Kisii, Matiang'i aliwaonya walimu wanaovunja sheria kwa kutumia mali ya umma kwa binafsi zao.

“Naomba kila mwalimu kuhakikisha shule yake imefanya vyema katika mitihani ya kitaifa na wale ambao hutumia mali ya serikali kujisomesha na kufanya shughuli zingine za binafsi nawaonya,” alisema Matiang’i.

Wakati huo, Matiangi alitoa onyo kali kwa walimu ambao hawafundishi wanafunzi kwa kutohudhuria madarasani huku akisema wizara yake haitakubali hilo kuendelea kufanyika kamwe.