Maduka ya kuuza vitabu na sare za shule yanaendelea kushuhudia ongezeko la wateja, hii ni baada ya wanafunzi kuendelea na matayarisho ya kurejerea masomo ya muhula wa kwanza baada ya likizo ya mwezi Desemba.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hata hivyo wanabiashara wengi wamehoji kuwa mauzo ya vitabu vya kusoma yameshuka kwa asilimia kubwa, baada ya walimu kuanza mgomo na kutatiza mipango ya wanafunzi kurejea shuleni

 Kulingana na wanabiashara hao, msimu wa shule kufunguliwa huwapa wateja wengi licha ya mfumo wa elimu bila Malipo, ambapo wanafunzi hupewa vitabu shuleni bila wazazi kugaramika.

Hata hivyo, mfanyibiashara John musyoka anayemiliki duka la vitabu na lingine la sare za shule amesema huenda biashara yao ikaimarika baada ya mapato ya chini mwaka jana.

Musyoka amedokeza kuwa biashara ya vitabu vya kusoma hupata wanunuzi wengi, huku akiongeza kuwa washikadau katika sekta ya elimu hununua vitabu pamoja na mitihani ya hapo awali ili kutahini wanafunzi wanapojiandaa katika mitihani ya kitaifa.

“Hatujakua na mapato ya kawaida kama nyakati zingine wanafunzi wanaporudi shuleni. Huu mgomo umehadhiri pakubwa kurudi kwa wanafunzi shuleni, na sisi pia tumehadhirika maana biashara iko chini,” alisema Musyoka.